Polisi wa KDF chini ya ulinzi baada ya kumnajisi mwanafunzi

Muhtasari
  • DCI yamtia mbaroni askari wa KDF aliyemnajisi mwanafunzi wa kidato cha kwanza siku ya jumanne
  • Kabura aliahidi msicha huyo,16,ambaye ni jamaa yake kumpleka shule bali hakutimiza ahadi yake
Pingu
Image: Radio Jambo

Afisa wa polisi wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya(KDF) ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi wa DCI baada ya kumnajisi msichana wa shule ambaye ni jamaa yake.

Kulingana na taarifa ya DCI askari huyo alifanya kitendo hicho alipomuahidi mtoto huyo kumpeleka shule ilhali akmpitishia kwa vyumba vya kulala Kiriaini na kumnajisi na kisha kuendelea na safari.

"Polisi wa kitengo cha KDF yuko chini ya ulinzi baada ya kumnajisi mwanafunzi wa kidato cha kwanza siku ya Jumanne,Spte Martin Kabura ambaye hufanya kazi katika eneo la Embakasi, alimuahidi mwanafunzi huyo kumpeleka shule eneo la Othaya 

 

Lakini alimpitishia kwanza katika vyumba vya kukondisha vya kulala katika eneo la Kiriaini na kumnajisi baadaye akaendelea na safari." Ilisoma Taarifa ya DCI.

Pia DCI ilisema kwamba msichana huyo alipelekwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Nyeri.

"Cha kusikitisha msichana huyo ni jamaa yake, na alikuwa amemuahidi kumpeleka shule,ahahdi ambayo hakutimiza 

Polisi waaliandamana na msichana huy hadi katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Nyeri ii akapimwe huku Kabura aiwa mikononi mwa polisi."