Ndege ya Boeing 737 ya Sriwijaya Air Indonesia, Jakarta yapoteza mawasiliano baada ya kupaa

Muhtasari
  • Ndege ya Boeing 737 indonesia yapoteza mawasiliano baada ya kupaa 
  • Ndege hiyo ilikuwa imewabeba zaidi ya abiria 60

Ndege inayokadiriwa kuwa na abiria 62 imepiteza mawasiliano muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Indonesia, Jakarta.

Maafisa wamesema kwamba Ndege hiyo ya kampuni ya Sriwijaya Air aina ya Boeing 737 imepoteza mawasiliano ilipokuwa inaelekea Pontianak magharibi mwa eneo la Kalimantan.

Mtandao unaofuatilia safari za ndege Flightradar24.com umesema ndege hiyo imepoteza mawasiliano baada ya kupaa mita 3,000 ndani ya dakika moja.

 

Wizara ya usafirishaji imesema shughuli za utafutaji na uokozi wa ndege hiyo zinaendelea.

Wizara hiyo imesema mawasiliano ya mwisho na ndege hiyo yalifanyika 14:40 saa za eneo.

Kulingana na taarifa za usajili, ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imetumika kwa miaka 27.

Shirika la ndege la Sriwijaya Air, limesema bado linakusanya taarifa kuhusu ndege hiyo.

Moja ya ajali hizo ilitokea Oktoba 2018, ikiwa ni ndege ya shirika la Indonesia Lion Air ambayo ilitumbukia baharini dakika 12 baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta na kusababisha vifo vya watu 189.