Nani aliwadanganya hoja ya kumbandua DP Ruto itaishi? Millicent Omonga auliza ANC

Muhtasari
  • Milicent Omanga azua gumzo mitandaoni baada ya kumtetea DP Ruto dhidi ya chama cha ANC
  • Chama hicho ambacho kimeongozwa na Musalia Mudavadi kilimsishi DP ajiuzulu la sivyo watambandua mamlakani

Seneta mteuliwa Millicent Omanga  amezua gumzo mitandaoni baada ya kuwathubutu wanachama cha ANC kumbandua naibu rais William Ruto mamlakani.

Hii ni baada ya chama hicho siku ya Jumanne kumwambia DP Ruto ajiuzulu la sivyo wako tayari kumbandua mamlakani.

Omanga amekuwa mwandani wa karibu wa naibu rais William Ruto, huku akipinga hoja ya wanachama hao.

Taarifa kutoka kwa naibu mwenyekiti wa chama hichi Ayub Savula ilisoma kama ifuatavyo

"Tanataka kuambia wakenya ukweli kuhusu Ruto, lakini pia tunamuita naibu rais afanye jambo sawa la kujiuzulu la sivyo atafutwa kazi

Kuelekea mwisho huu, tumeongoza katika kuandaa hoja ya kumbandua mamlakani, ili kuwalinda wakenya dhidi ya vurugu ilichachishwa kwa siri na Ruto

mtu tajiri na mwenye nguvu serikalini akijifanya maskini." Taarifa Ilisoma.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter wa Millicent Omanga alikashifu chama hicho huku ujumbe wake ukiibua gumzo kwenye mitandao hiyo.

"Eti @anc_party  wanataka kuanzisha hoja ya kumbandua mamlakani naibu rais wa jamhuri ya kenya Nani hata aliwadanganya hoja kama hiyo ingeweza kuishi?" Aliuliza Millicent.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya waliozua gumzo kwa ajili ya ujumbe wake seneta huyo.

 

Catherine Chepkoech: Let me remind you when you appeared before the Jubilee Party disciplinary committee, they asked you hard questions and you started farthing.

victormzachary: nyani haoni kundule alisahau

Nelson Buchila: Hivyo ndyo mulichocha sonko mukaenda momabsa mukamwagiwa pesa impeachment ilifanyika roho Safi tena muunze that's why kenyan is a democratic country shkuru mungu wewe unjua n votes ngapi mtu yafa kupta awe mca, senator,relax it's not easy how you think

Francis Odipo: Ayub Savula is just a messenger,the impeachment motion if brought today I assure you it will sail through by a landslide margin 

richard: we have numbers madam.......sasa tumeamua huyo mwizi aende sugoi...we cannot trust him anymore

Onyancha oburu : all impeachment motions have passed if they have blessings of Uhuru and Raila