Aliyekuwa mkewe Johnstone Muthama,Agnes Kavindu kuwania kiti cha useneta Machakos

Muhtasari
  • Aliyekuwa mkewe Johnstone Muthama,Agnes Kavindu kuwania kiti cha useneta Machakos
  • Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alisema kwamba ana imani kwamba Agnes ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho

Chama cha Wiper kimemteua Agnes Kavindu kuwania useneta wa Machakos  hii ni kufuatia  kifo cha aliyekuwa Seneta Bonface Kabaka.

Ni uchaguzi utakao fanyika tarehe 18 Machi mwaka huu.

Kavindu alikuwa mkewe aliyekuwa seneta wa kaunti hiyo Johnstone Muthama na alikabidhiwa cheti cha Wiper na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.

 

Kalonzo aliwataka viongozi wote wa Ukambani kumpigia debe Kavindu ili aibuke mshindi kwenye uchaguzi huo mdogo.

Wakati huo huo kinara huyo wa wiper alimshtaki naibu rais William Ruto kwa unafiki.

"Nani hajui kwamba rais Uhuru Kenyatta alipata asilimia 50 ya serikali, na naibu wake William Ruto akapata asilimia 50 ya serikali

Angalau uteuzi wake rais ulionyesha kiongozi wa kitaifa, Nina imani kuwa Kavindu ndiye ataibuka kuwa seneta wa Machakos." Kalonzo Alizungumza.