Wakili Elizabeth Koki aliaga dunia kwa kukosa hewa-Upasuaji waonyesha

Muhtasari
  • Upasuaji wa mwili wake Elizabeth waonyesha alinyongwa hadi kifo
  • Wakili Elizabeth alipatikana ameaga dunia nyumbani kwake Ijumaa Januari 8
Marehemu wakili Elizabeth Koki.
Marehemu wakili Elizabeth Koki.
Image: CORAZON WAFULA

Upasuaji ambo ulifanywa kwa mwili wa mwendazake wakili Elizabeth Koki ambaye alipatikana ameaga dunia Ijumaa, Januari 8 ulionyesha kwamba aliaga dunia kwa kukosa hewa.

Hii ni kulingana na ripoti ya upasuaji ambao ulifanywa na mtaalam wa upasuaji Johansen Oduor.

Pia ripoti hiyo ilionyesha kwamba mwendazake alikuwa na majeraha kwenye mdomo wake 

 
 

"Alikabwa shingo hadi kifo." Mtaalam huyo aliambia people daily.

Inadaiwa kwamba wawili hao walianza kekeleleshana baada ya wakili huyo kupata picha ya mwanamke kwenye simu ya mpenzi wake Christian Kadima.

Usiku wa kukumbana na kifo chake Kadima aliambia maafisa wa polisi kwamba Koki alikuwa amemuita nyumbani kwake Syokimau ili kuzungumza kuhusu picha hiyo.

Mshukiwa wa mauaji ya wakili Elizabeth Koki, Christian Kadima alifikishwa katika mahakama ya Mavoko siku ya Jumatatu.
Mshukiwa wa mauaji ya wakili Elizabeth Koki, Christian Kadima alifikishwa katika mahakama ya Mavoko siku ya Jumatatu.
Image: GEORGE OWITI

Uchunguzi pia ulifichua kwamba wawili hao wamekuwa wakipigana kwa muda sasa kabla ya Koki kuaga dunia.

Kadima alidai kwamba mwendazake aligonga ukuta na kichwa chake, huku uchunguzi na upasuaji wa mwili ukionyesha kwamba alinyongwa hadi akafariki.

"Mshukiwa mkuu amehojiwa na kulingana na mambo inaonekana wawili walikuwa wanapigana kwa muda na walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi." Alisema mpelelezi.

Pia jamaa wa karibu wa Kadima alidai kwamba walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya harusi ya wawili hao huku wakifikishiwa habari za kifo chake Koki.