Uchaguzi Uganda: Museveni atangazwa mshindi wa kura ya urais

Museveni
Rais Yoweri Museveni Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ndiye aliyetangazwa mshindi wa kura ya urais siku ya Jumamosi.

Mpinzani wake mkuu Bobi Wine alidai udanganyifu ulienea na akasema raia wanapaswa kukataa matokeo hayo.

Museveni alishinda kura milioni 5.85, au asilimia 58.6, wakati mgombea mkuu wa upinzani Wine akipata na kura milioni 3.48 (34.8%), Tume ya Uchaguzi ilisema katika mkutano wa waandishi wa habari hyku wakitangaza matokeo ya mwishoya uchaguzi huo uliofanyika Alhamisi.

Hapo awali, Wine alimshtaki Museveni kwa kubuni matokeo na aliita uchaguzi huo "uchaguzi ulio na udanganyifu zaidi katika historia ya Uganda".

Katika mahojiano ya simu kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwa, aliwahimiza raia kukataa matokeo. Wine, mwimbaji aliyegeuka kuwa mbunge, pia alisema nyumba yake katika mji mkuu, Kampala, ilizungukwa na mamia ya wanajeshi na kwamba jeshi halimruhusu aondoke.