Afisa wa KDF ajaribu kulipua gruneti nyumbani kwa mewe wa zamani

Afisa mmoja wa KDF atafikishwa mahakamani kesho kwa madai ya kujairbu kutumia gruneti la moshi nyumbani kwa mkewe wa zamani katika eneo la Marachi Central kaunti ya Busia.

DCI inasema afisa huyo Denis Ochieng alifanya kitendo hicho kufuatia mgogoro kuhusu malezi ya mtoto.

hayo yakijiri, imebainika kuwa Lawrence Warunge, mwanafunzi wa chuo kikuu aliyekiri kuwaua jamaa zake wanne na mfanyikazi mmoja wa nyumbani katika eneo la Karura , kaunti ya Kiambu ana utimamu wa akili kwa hivyo ana uwezo wa kuhukumiwa.

Iwapo atakubali makosa yake, atakumbushwa kuhusu matokeo ya vitendo vyake kabla ya mahakama kuamua itakapotoa uamuzi wake. Jamaa hao wanne walizikwa nyumbani kwao.

kwingineko, kinara wa ODM Raila Odinga amemshutumu naibu rais William Ruto kwa unafiki. Raila  anasema Ruto hafai kuzungumza kana kwamba hahusiki na serikali anapofanya kampeni zake za mwaka 2022 za urais.

Tukielekea pwani, mbunge wa Likoni Mishi Mboko anasema baadhi ya maafisa wa polisi wanahusika na ulanguzi wa mihadarati mjini Mombasa. Mboko anadai kuwa maafisa hawa hupokea hongo ili kuwalinda walanguzi wa dawa za kulevya na wanastahili kushtakiwa.