Covid-19: 30 wamelazwa ICU, watatu waaga dunia

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

 

Watu thelathini wanao ugua virusi vya Corona wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi kufikia Jumapili ya leo.

Waziri wa afya Kagwe Mutahi alithibitisha kuwa watu 80 zaidi wamepatikana na ugonjwa huo kutokana na sampuli 3,733 zilizopimwa masaa 24 yaliyopita.

Hii inamaanisha kuwa kufikia sasa asilimia 2.4 ya wakenya ndio wamepatikana na ugonjwa huo.

Kesi hizo mpya zinahusisha wakenya 62 na wageni 18 walio na kati ya umri wa miezi 11 hadi miaka 81.

Hata hivyo, idadi ya vifo imezidi kupanda baada ya wagonjwa watatu kuaga dunia kutokana na virusi hivyo.

Idadi ya wakenya waliopoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo ni 1,731.