Leicester ililaza Southampton 2-0 kupitia magoli ya James Madison na Harvey Barnes katika kipindi cha kwanza na kuhakikisha wamepanda hadi nafasi ya pili kwenye jedwali ya EPL, alama moja nyuma ya Manchester United.
Kwingineko, Chelsea ililaza Fulham 1-0 na kupanda hadi nafasi ya saba kwenye jedwali kupitia goli la pekee la Mason Mount katika kipindi cha pili.
Katika matokeo mengine jana, Westham ililaza Burnley 1-0 huku Leeds pia wakinyukwa 1-0 na Brighton, nao Wolves walipoteza 3-2 dhidi ya Westbrom, huku kocha Sammy Allardyce akinyakua ushindi wake wa kwanza tangu kuchukua usukani mwezi uliopita.
Na Katika ligi kuu ya FKF Humu nchini, Tusker ilibwaga Kariobangi Sharks 4-2 na kupanda hadi nafasi ya pili alama moja nyuma ya viongozi KCB, huku Bandari nao wakipanda hadi nafasi ya nne baada ya kuwalaza Kalamega Homeboyz 4-3 ugani Mbaraki.
Kwingineko Nzoia Sugar ilinyuka Sofapaka 2-1 na kandikisha ushindi wao wa kwanza msimu huku wanajeshi Ulinzi wakitoka sare ya 1-1 na City Stars.
Katika tetesi za soka duniani,Mesut Ozil yuko mbioni kuondoka ugani Emirates baada ya kuchezea Arsenali kwa muda wa miaka saba.
Mzaliwa huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32 amekubali kujiunga na miamba wa Uturuki Fenerbahce kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Ozil hakua katika mipango ya kocha mkuu Mikel Arteta licha ya uzoefu wake na hajacheza mechi yoyote msimu huu.
Kwa mujibu wa Fernabache, the gunners watalipa marupurupu ya Ozil kwa miezi sita kama walivyokubaliana. Kwingineko, Nyota wa Bayern Munich Kingsley anadai yuko sawa katika ligi ya Bundesliga, na hatoondoka licha ya kuhusishwa na miamba wa Uingereza Manchester United na Man City.
Kiungo huyo wa Ufaransa amekua katika hali dhabiti huku akifunga magoli matano na kusaidia kufunga tisa, katika mechi 15.
United wamekua wakimmezea mate Kingsley kwa muda mrefu na huku Manchester City pia wakionyesha nia ya kumsajili.