Lupita Nyong'o amkejeli CS Balala baada ya kusema hawakumpata kwa miaka 5

Muhtasari
  • Lupita acheka madai yake waziri wa utalii Balala
  • Balala alisema kuwa wamekuwa wakimtafuta Lupita kwa miaka mitano
Lupita
Image: Hisani

Mwigizaji wa Kenya aliyeshinda tuzo tofauti Lupita Nyong’o amecheka madai kwamba Kenya imekuwa ikimtafuta kwa miaka mitano.

Waziri wa Utalii Najib Balala alisema haya baada ya kulazimishwa kutetea uteuzi wa hivi karibuni wa supermodel Naomi Campbell kama balozi wa kimataifa wa Magical Kenya badala ya Lupita.

Balala aliliambia Nation kwamba wizara yake ilijaribu kuwasiliana bila mafanikio na Lupita kwa miaka mitano sasa.

“Najua kila mtu anauliza kwanini asiulize Lupita. Lupita ana ahadi na mameneja wake hawawezi kuturuhusu kumfikia. Tumetumia miaka mitano iliyopita kumtafuta Lupita." Balal Alisema.

Baada ya kuona na kusikia madai yake Balala Lupita alipakia picha kwenye ukurasa wake watwitter huku akicheka madai yake Balala.

"Mimi nikisikia Wizara ya Utalii ya Kenya imekuwa ikinitafuta kwa miaka mitano. #Imrightherebaby #alternativefacts." Aliandika Lupita.