Hofu kutanda kaunti ya Kisii baada ya zaidi ya makanisa 5 kuchomwa na watu wasiojulikana

Muhtasari
  • Zaidi ya manisa 5 yachomwa kaunti ya kisii na watu wasiojulikana
  • Waumini sasa wanataka serikali kuingilia kati ili kubaini chanzo cha mioto hiyo
  • Wasimamizi wa maknisa hayo walisema kwamba wahalifu hao walivunja madirisha ya makanisa hayo

HABARI NA Elder Magati Obebo

Hofu imeendelea kutanda katika sehemu ya Otamba mji wa Janibu kaunti ya Kisii, baada ya kanisa moja zaidi kuchomwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo

Kwa wiki moja sasa zaidi ya makanisa matano yamechomwa nyakati za usiku na watu wasiojulikana.

 

Leo asubuhi waumini wa kanisa la Otamba Pag waliamkia kisa cha madhabau ya kanisa lao yamechomwa.

Wasimamizi wa kanisa hilo walisema kwamba waliotekeleza kisa hicho walivunja madirisha.

Linaloshangaza katika matukio yote haya ni kuwa sehemu za madhabau tu ndizo zinateketezwa.

Aidha makabati ya kuweka nyaraka za kanisa yalichomwa, kufikia leo madhabau katika makanisamawili ya katoliki,moja la kiadventista na sabato na matatu ya kiroho yameathirika katika wimbi la kuchoma makanisa.

Waumini sasa wanataka serikali kuingilia kati na kubaini chanzo za mioto hiyo