Vijana wavuruga Mkutano wa kinara wa ODM Raila Odinga Githurai

Muhtasari
  • Vijana wavuruga Mkutano wa ODM Raila Odinga Githurai huku wakiimba kauli mbiu ya Hustler
  • Raila alianza mkutano wake katika eneo la Roysambu alipowaeleza watu umuhimu wa BBI kabla ya kuelekea Githurai

Kinara wa ODM Raila Odinga Jumatano Januari 27 aliingia soko la Githurai kwa kishindo katika kampeni zake kuhubiri mswada wa BBI. 

Hotuba ya kiongozi wa ODM Raila Odinga huko Githurai Jumatano ilikatizwa na vijana wakiimba kaulimbiu za 'hustler'.

Raila amekuwa kwenye kampeni ya kuipongeza BBI wakati inaelekea kwa mabunge ya kaunti baada ya wakala wa uchaguzi Jumanne kudhibitisha saini zaidi ya milioni moja zilithibitishwa kama zinaunga mkono muswada huo.

Huko Githurai, kulikuwa na polisi nzito na vijana walirudishwa nyuma na vijana wa pro -Raila.

Kikundi cha hustler kiliamua kutupa mawe kwa msafara wa Raila na kuendelea kuimba "Ruto na hustler" karibu mita 50 kutoka ambapo mkuu wa upinzani alikuwa akihutubia wafuasi.

Polisi walitumia vitoa machozi ili kuwatawanya vijana hao, walipokuwa wanapenya kuenda mahali Raila alikuwa nahutubia umati.

Raila alianza hotuba zake katika eneo la Roysambu ambapo alihutubia umati na kuwaelezea umuhimu wa BBI.