Shirika la Kenya national qualifications authority limezindua mbinu ya kudhibitisha vyeti bandia

Muhtasari
  • Shirika la Kenya national qualifications authority limezindua mbinu ya kudhibitisha vyeti bhandia

Wakenya Sasa wanaweza kuripoti vyeti bhandia kupitia mtandaoni . Katika njia hii mpya mtu yeyote anaweza tumia tovuti kuripoti visa vya vyeti bandia kupitia tovuti rev@knqa.go.ke/cheti-mwitu.

Kwa mujibu wa mkurungezi mkuu wa Shirika hilo Bwana Juma Mukhwana,njia hii itawezesha kumaliza vyeti bhandia vya masomo humu nchini

Watu nchini wamekuwa wakipata vyeti bandia kama vile vyeti vya shule mara kwa mara.

Mkurugenzi Juma alisema kwamba baada ya mtu kuripoti kuwa kyeti chake kimeibiwa na  kutumiwa na mtu mwingine watachunguza madai hayo kwa kina.

"Tumezindua mbinu ya kuthibitisha vyeti bandia inayofahamika kama 'Vyeti mwitu, mtu anaweza ripoti kupitia kwenye tovuti na kisha tutachunguza zaidi

Itasaidia pia watu kugundua vyeti bandia," Alisema JUma.