Kuna watu wataachwa mtaani, Raila na Ruto wakifanya kazi pamoja kabla ya uchaguzi mkuu-Kuria

Muhtasari
  • Moses KUria adai Raila na Ruto watafanya kazi pamoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022
  • Jumapili Kalonzo alidai kwamba haitaji idhini ya mtu yeyote bali anahitaji idhini yake Mungu
Moses Kuria

Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria kwa ujasiri sana alisema kwamba aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga na naibu wake rais William Ruto watafanya kazi pamoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Huku akiwa kwenye mahojiano mwanasiasa huyo alidai kwamba kuna baadhi ya wanasiasa ambao watawachwa mtaani baada ya wawili hao kuungana mkono.

"Raila Odinga na William Ruto watafanya kazi pamoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 na kuna watu watawachwa kwa mataa

 

"Risasi ya mwisho ya ukweli na unajua Baba, amekuwa katika upinzani katika maisha yake yote lakini yeye yuko kwenye kona nzuri ya upinzani, si iko iko na baridi," Alisema Kuria.

Matamashi yake Kuria yanajiri siku chache baada ya kinara wa chapa cha Wiper Kalonzo Musyoka pamoja na Moses Wetangula, Mudavadi kumpa vijembe kinara wa ODM Raila.

Jumapili Kalonzo alidai kwamba haitaji idhini ya mtu yeyote bali anahitaji idhini yake Mungu.