'Kuna Mungu mbinguni,'Sonko azungumza baada ya kuachiliwa kwa dhamana

Muhtasari
  • Sonko azungumza baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya shillingi milioni moja
  • Kupitia kwenye ujumbe wake alisema kwamba kuna Mungu mbinguni ambaye anasikia na kujibu maombi
  • Sonko aliwashukuru wote ambao wamekuwa wakimuombea wakati wake mgumu
sonko
sonko

Gavamna wa zamani Mike Sonko hatimaye ameungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuachiliwa kwa dhamana na shilingi milioni moja.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Sonko aliwashukuru wote ambao walimuombea alipokuwa kwenye shida.

"Kuna Mungu mbinguni anaye sikia na kujibu maombi, Haijalishi kanisa hili ni kubwa au ndogo kiasi gani, iwe katika makazi duni au sehemu yoyote ya Kenya, nataka tu kukushukuru sana kwa kuniombea kuachiliwa.

Nitakuja kushirikiana nawe mara zote nitakapopona kabisa na kuruhusiwa kutoka hospitalini. Nataka pia kuwashukuru wale wote ambao walikuwa wakiniombea iwe kutoka kwa makanisa tofauti, misikiti au mahekalu ya dini.

Endelea kuniombea na Mungu Atanisimamia kushinda shida zote kwani ana mipango ya kunifanikisha na sio kunidhuru, mipango ya kunipa tumaini na siku zijazo. Mungu Akubariki Wote," Aliandika Sonko.

Maneno ya Sonko yalikuja masaa kadhaa baada ya kuachiliwa na Korti ya Kupambana na Ugaidi huko Kahawa Magharibi kwa dhamana ya shillingi milioni moja na mdhamini sawa, baada ya kukana makosa manne yanayohusiana na ugaidi.