Rashid Echesa kuonekana kama hatari na mhalifu-IG Mutyambai

Muhtasari
  • Mutyambai asema Echesa ataonekana mhalifu asipojisalimisha katika kituo cha polisi kilicho karibu naye
  • Echesa alipatikana na hatia kwa kumpiga afisa wa IEBC wakati wa uchaguzi wa Matungu
Aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa
Aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa
Image: MERCY MUMO

Waziri wa zamani wa michezo Rashid Echesa ataonekana kuwa kama mhalifu wa hatari ikiwa hatajisalaimisha kwa DCI polisi wamesema.

Mkaguzi Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai siku ya Ijumaa alisema wamempa Echesa ambaye yuko mafichoni mpasa saa saba mchana  kujisisalimisha mwenyewe.

Echesa alipatikana na hatia kwa kumpiga afisa wa IEBC wakati wa uchaguzi wa Matungu.

 

Hii ilitokea baada ya kudai kwamba afisa huyo wa IEBC Peter Okura alikuwa anawazui wakala wao kushuhudia wananchi wakipiga kura.

"Sheria Inasema Kuwachagua mawakala lazima shahidi kupiga kura!

Kupitia video iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii afisa huyo wa IEBC alisikika akijitetea akisema kwamba alikuwa akifuata maelekezo. 

Lakini kabla ya kumaliza kuzungumza, Echesa akampiga. Kisha akaingia mafichoni baada ya polisi kuagizwa wamkamate kwa ajili ya kitendo chake.

"Echesa ana mpaka Ijumaa alasiri kutoa ripoti kwenye kituo cha polisi cha karibukwa kumpiga afisa wa IEBC huki Matungu," taarifa kutoka kwa msemaji wa polisi Charles Owino ilisoma.

"IG amemwagiza Rashid Echesa ambaye yuko mbioni baada ya kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kujisalimisha kwa Kituo cha Polisi kilicho karibu saa 1.00 jioni leo vinginevyo atachukuliwa kama mhalifu mwenye silaha na hatari," alisema

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pia amedai kukamatwa kwa Echesa akisema angepaswa kuandikisha ripoti hiyo badala ya kumpiga afisa huyo.

 

Mutyambai aliwalelekeza polisi kuwashtaki wabunge waliokamatwa wakati wa machafuko huko Kabuchai.

Wabunge hao ni pamoja na Samson Cherargei, Nelson Koech, Didmus Barasa na Wilson Kogo.

Wabunge walilala katika  kituo cha polisi cha Bungoma.