Noordin Haji awapa polisi siku 30 kuwasilisha ripoti juu ya vurugu vilivyotokea Alhamisi

Muhtasari
  • Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amewapa polisi siku 30 kuwasilisha ripoti juu ya uchaguzi mdogo uliomalizika
  • Haji pia aliwaambia polisi kuwasilisha ripoti ya uchunguzi juu ya madai kwamba waziri wa zamani wa Michezo alishambulia afisa wa IEBC

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amewapa polisi siku 30 kuwasilisha ripoti juu ya uchaguzi mdogo uliomalizika.

Katika barua kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai, Haji alisema ripoti hiyo inapaswa kunasa visa vyote vya ghasia na vitendo vingine vibaya vya uchaguzi haswa katika eneo bunge la Matungu ndani ya kaunti ya Kakamega na Kata ya London katika Kaunti ya Nakuru.

Haji pia aliwaambia polisi kuwasilisha ripoti ya uchunguzi juu ya madai kwamba waziri wa zamani wa Michezo alishambulia afisa wa IEBC.

 

"Ninaagiza kwamba mara moja uchunguzi  uanzishwe wa pamoja juu ya madai hayo ya vurugu na uwasilishendani ya siku 30," Haji alisema.

Agizo la Haji linakuja siku moja baada ya Mutyambai kuwaamuru polisi kuwashtaki wanasiasa wote waliokamatwa kutokana na vurugu hizo.

Wabunge hao wanne ambao ni washirika wa karibu wa Naibu Rais William Ruto waliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 taslimu baada ya kukaa usiku katika seli za polisi.

Wanasiasa hao ni pamoja na Seneta wa Nandi Samson Cherargei, Didimus Barasa wa Kimilili, Wilson Kogo wa Chesumei na Nelson Koech wa Belgut.

Wabunge walikamatwa kwa madai ya kufadhili vurugu katika uchaguzi mdogo uliomalizika, siku ya Alhamisi huko Matungu na london.

Wote walikana mashtaka na kesi hiyo ikisikilizwa Aprili 4.