Sikujua DJ atasimamisha reggae mwenyewe-Moses Kuria

Muhtasari
  • Moses Kuria asema haya kuhusu BBI, huku akidai alijua tu Mungu pekee ndio anaweza simamisha reggae
  • BBI ilizinduliwa na rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga mwaka jana, huku baadhi ya wanasiasa wakipinga hatua hiyo
  • Zaidi ya kaunti 40 zilipitisha ripoti ya BBI huku baadhi ya kaunti zingine zikipiga teke mchakato huo
Moses Kuria

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amewaacha wanakenya na mdahalo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba Raila amesimamisha Reggae.

Kuria amekuwa mwandani wa karibu wa naibu rais William Ruto, huku akipinga mchakato wa maridhiano BBI.

BBI ilizinduliwa na rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga mwaka jana, huku baadhi ya wanasiasa wakipinga hatua hiyo.

 

Zaidi ya kaunti 40 zilipitisha ripoti ya BBI huku baadhi ya kaunti zingine zikipiga teke mchakato huo.

Ni mchakato ambao ulikusanyishiwa saini, huku kura ya maamuzi ikisubiriwa kufanyika.

Kuria kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alidai kwamba Raila amesimamisha Reggae, na alijua kwamba ni Mungu tu peke yake anaweza simamisha mchakato huo.

"Niliishi kujua kwamba mungu na mtu mwingine ndio wanaweza simamisha Reggae,lakini sikujua kwamba DJ atasimamisha reggae mwenyewe," Kuria aliandika.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya;

Magufuli Benjamin: When baba is happy we are happy

Cally Muya: It's so heartbreaking that Uhuru is Betraying ODM a time when they were so much desperate for Ruto's impeachment..

 

Gachoki Jn: And yet mcas passed the bill overwhelmingly to punish Ruto. Little knowledge is dangerous

Kennedy Macharia: After BBI handshake will be done. ODM knows very well their relations with uhuru is coming to an ultimate end.To energize their campaign they have to compel uhuru and buy time. Remember timing is everything in politics.ODM is just a shell party riding on BBI agenda, nothing new,it's as well as dead.They haven't participated in government checks and watchdog.No selling point coming election.Machoos😭

Dan Baraza: Chungwa zimetoshea wheelbarrow. Fans of Raila and Ruto after fighting each other, how will this feel 😂😂😂