Mwanamuziki azuiliwa kwa siku 10, kwa kifo cha mumewe

Muhtasari
  • Korti iliruhusu polisi kumzuilia kwa siku 10, mjane wa askari wa Kikosi cha Ulinzi cha Kenya ambaye alikufa wakati wa mabishano makali katika makazi yao Kahawa Wendani, kaunti ya Kiambu

Korti iliruhusu polisi kumzuilia kwa siku 10, mjane wa askari wa Kikosi cha Ulinzi cha Kenya ambaye alikufa wakati wa mabishano makali katika makazi yao Kahawa Wendani, kaunti ya Kiambu.

Hii itawezesha polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Pia itawezesha mashirika kufanya uchunguzi wa mwili wa Daniel Onyango Jumatano ili kujua jinsi alivyokufa.

Mjane huyo, Violet Asale, alifikishwa mbele ya korti ya Kiambu Jumanne wakati polisi walitoa ombi tofauti ya kumzuilia wakati wanaendesha uchunguzi wa kifo.

Asale ni mwanamuziki anayeenda kwa jina Zian Achama.

Baadhi ya nyimbo zake ni pamoja na 'Nimechoka', 'I Love You', 'Falling in Love' na 'Gimme Love'.

Korti ilipunguza siku zilizoombwa kutoka 15 hadi 10.

Asale amewaambia polisi mumewe alikuwa na shida ya kupumua na hakumng'ata hadi kufa, kama ilivyoripotiwa.

Aliongeza alijiumiza ndani ya nyumba walipokuwa wakizozana Jumamosi karibu usiku wa manane.

Aliwaambia polisi mumewe alitoka nje ya chumba chao baada ya mabishano, akisema hawezi kupumua.

"Mwanamke huyo anasema hakutumia silaha yoyote. Anadai kwamba mwanamume huyo alijaribu kumnyonga kabla ya kupigana na kukimbia nje ya chumba chao cha kulala," afisa aliyefahamu uchunguzi huo aliiambia Star.

"Muda mfupi baadaye Daniel  alitoka nje akilalamika juu ya kutoweza kupumua. Lakini tutajua zaidi," akaongeza.

Alisema Onyango alimng'ata mgongoni, na kumfanya amuume. Alimuuma katika kifua, bega na kidole gumba.