Covid-19: Watu 1,030 wapatikana na virusi huku 21 wakiaga dunia

Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Hivi leo watu 1,030 wamepatikana na virusi vya Corona kutokana na sampuli 8,316 zilizopimwa katika masaa 24 yaliyopita.

Kutokana na visa hivyo watu 995 nu wakenya huku 35 wakiwa wageni.532 ni wanaume huku wagonwa 498 wakiwa wanawake.

Mgonjwa mchanga zaidi ana miezi kumi huku mkongwe zaidi akiwa na miaka 99.kufikia sasa ni watu 145,184 waliopatikana na virusi hivyo kutokana na vipimo 1,557,704.

Hata hivyo, wagonjwa 422 wamepata nafuu, 105 kutoka vituo vya afya huku 317 wakipata nafuu wakiwa manyumbani mwao.Idadi ya watu waliopata nafuu imefikia 98,605 kufikia sasa.

Hata hivyo katika hali ya kutamausha, watu 21, wamepoteza maisha yao katika masaa 24 yaliyopita.

Wagonjwa 1,616 wamelazwa katika vituo mbalimbali vya afya huku wagonjwa 4,243 wakiwa manyumbani mwao.Kati ya hao, 247 wako katika vyumba vya wagonwa mahututi.