'Jiwe letu' Wanawe Akothee wamsherehekea kwenye siku yake ya kuzaliwa

akoth
akoth

Hii leo, mwanabiashara na msanii mashuhuri nchini, Akothee anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Akothee anaadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa.

Siku hii maalum inajia siku kadhaa tu baada yake kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe Prince Oyoo. Kwa kweli mwezi wa nne ni wenye furaha na sherehe katika nyumba ya madam boss.

Kupitia mitandao yao ya kijamii, wanawe madam boss, Vesha na Rue Baby wamemsherehekea mama yao kama jiwe kuu katika maisha yao, huku wakimtaja kama nguzo ya baraka mioyoni mwao.

 

Kifungua mimba wake, Vesha Okello aliandika;

Heri ya kuzaliwa mwamba wangu @akotheekenya nakupenda sana unapozeeka leo nataka ujue tu kuwa wewe ni baraka ya kweli heri ya kuzaliwa mpenzi wangu.

Kwa upande wake, Rue Baby alimtakia mamake ambaye ni rafikiye wa dhati heri ya siku ya kuzaliwa na kumtakia baraka chungu nzima.

Aliandika;

Heri ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yangu wa karibu. SIBUOR MADHAKO ❤❤❤🔥. Nakupenda mama. Unapo ongeza mwaka mwingine maishani na uwe na baraka juu ya baraka. Kuwa na siku ya kufana mpenzi wangu. @akotheekenya

Tunamtakia madam boss Akothee siku njema yenye furaha na baraka chungu nzima.