Picha: Kutana na mwanaume anaye yeyusha moyo wake Yvette Obura

Siku kadhaa zilizopita, kidosho, Yvette Obura alichapisha picha ya pete ya almasi, akithibitisha kuwa tayari amempata mchumba na yuko tayari kuolewa.

Jina la kipenzi chake ni kijana mtanashati, Trevor Nzomo. 

Obura ni mamake mzazi mwanawe wa msanii Bahati, Mueni.

Katika picha hiyo aliyochapisha katika mtandao wake wa Instagram, Obura alijifanya kuwa alikuwa akiwaonesha mashabiki wake jinsi kucha zake zilivyorembeka, lakini mashabiki wake moja kwa moja wakagundua pete ile na kumpongeza kwa kishindo.

Hata hivyo swali la wengi ni je, nani huyu kampata kidosho maidadi hivi?

Ikumbukwe kuwa mwezi wa pili mwaka huu, Yvette aliambatana na mpenziwe, Trevor katika studio za Radio Jambo katika mahojiano ya moja kwa moja, ambapo alifichua kuwa hana nia ya kuchapisha uso wake katika mtandao wa kijamii.

Hata hivyo, tumeweza kupata picha zake.

Tazama picha zifuatazo;

Trevor Nzomo. Mchumba wake Yvette Obura. Picha: Hisani