Bunge kuhoji kaunti kuhusu matumizi ya michango ya pesa za Covid-19

Lusaka
Lusaka

Bunge katika wiki zijazo litahoji wakuu wa kaunti kuhusu matumizi ya michango ya mabilioni ya pesa za  Covid-19. Spika Ken Lusaka anasema ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali imehusisha kaunti kadhaa ambazo hazina kumbukumbu za jinsi michango na fedha zilivyotumiwa.

Seneta wa Bungoma Moses Wetangula amehoji amri ya  kufungwa kwa kaunti 5 na kushindwa kutekeleza zoezi la kuchanja watu wengi dhidi ya Covid-19. Wetangula amehimiza Wizara ya Afya kuondoa marufuku ya kuingizwa kwa chanjo ya Sputnik ili kupiga jeki AstraZeneca na kusaidia katika kuwachanja wakenya wengi.

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amewataka Wakenya kupuuza propaganda zinazoenezwa kwa mitandao ya kijamii kuhusu chanjo ya Covid-19. Kalonzo anasema chanjo inabaki kuwa matumaini makubwa dhidi ya covid.

Kenya na Tanzania zimeanza shughuli ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ambao uliharibika kidogo.

Rais Samia Suluhu alisema jana baada ya kukutana na mjumbe maalum wa Kenya jijini Dar es Salaam kwamba utawala wake umeazimia kutatua baadhi ya masuala yaliyopo kati ya mataifa hayo mawili.