Familia ya kocha wa zamani wa raga Benjamin Ayimba yaomba msaada

Benjamin ayimba aomba msaada
Benjamin ayimba aomba msaada

Familia ya kocha wa zamani wa timu ya raga ya Kenya sevens Benjamin Ayimba imetuma ombi kwa wananchi kusaidia katika mchango wa kulipwa bili yake ya hospitali inayofikia millioni mbili sasa.

Ayimba alilazwa katika hospitali moja mjini Nairobi na ugonjwa wa celebral malaria tangu Disemba 2020.

Kocha huyo mzoefu aliongoza Shujaa kunyakua taji la Singapore sevens mwaka wa 2016 na pia aliwaongoza katika Olimpiki za Brazil.

Pesa zinaweza kutumwa kupitia  bill number 8021673.

Watu mashuhuri, jamaa na marafiki zake Ayimba wamekuwa wakichapisha jumbe za kuwajulisha wakenya hali yake Ayimba huku wakiungana kuomba msaada wa kulipa bili yake.