Seneta mteule Millicent Omanga alazwa hospitalini

Seneta mteule Millicent Omanga almaarufu 'Mama miradi' amelazwa hospitalini.

Seneta huyo alichapisha picha akiwa hospitalini, katika mtandao wake wa Instagram huku akiandika aya ya bibilia kuhusu uponyaji ila hakueleza ni kiini cha kuugua.

"Yeremia 30:17. Lakini nitakurejeshea afya yako, nitakuponya vidonda vyako, asema Bwana. Udhaifu wetu wote ni fursa tu kwa Mungu kuonyesha kazi yake ya neema ndani yetu. Amefanya hivyo kwa ajili yangu, Shika imani." Aliandika Mheshimiwa Omanga.

Soma jumbe za heri njema kutoka na mashabiki wake waliomuombea uponyaji.

Wagurah: Godspeed recovery Senator.

Eddie: Quick recovery Mom

Roberto: Quick recovery we 🙏 for you be strong 💪 we love you

Lemis Diana: Quick recovery Mama Miradi😢

Ugua upole mama miradi.