Covid-19:Watu 981 wapatikana na corona,26 waaga dunia

Muhtasari
  • Mtoto wa siku 7 miongoni mwa walioambukizwa corona
  • Watu 981 wapatikana na corona,26 waaga dunia
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 981 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 7,529katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 148,128 kutoka kwa sampuli 1,578,773.

Katika visa hivi vipya, 961 ni raia wa Kenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni, 563 ni wa kiume na 418 ni wanawake.

 

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana siku 7 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 97.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 665 wamepona virusi vya corona, 528 walipona wakiwa nyumbani huku 137 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 100,245 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 26 dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,420 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,623 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 5,565 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 269 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)