Picha ya siku: DJ Mo amzawadi Size 8 na gari jipya

 

Mcheza santuri mashuhuri, DJ Mo amezidi kuthibitisha upendo wake kwa mkewe msanii Size 8 baada ya kumzawadi na gari jipya.

Kupitia mtandao wake, DJ Mo alisema kuwa hiyo ilikuwa kama ishara ya kumpongeza mkewe ambaye hivi majuzi ameweza kutawala woga wake wa kuendesha gari. 

"Ninapenda magari sana na sasa kwa kuwa mke wangu ameshinda woga wa kuendesha gari, nataka afurahie Toy hii nzuri .. Ilinibidi nirembeshe gari hili kwa ajili ya mpenzi wangu ili aweze kuboresha ustadi wake wa kuendesha gari." Aliandika DJ Mo.

Hili lajia siku chache tu baada ya Size 8 kuchapisha kanda akionesha ustadi wake kama dereva.

Akisherehekea ushindi huo, Size 8 aliandika;

Nilishinda woga jamani HALLELUJAH kwa damu ya Yesu nilishinda woga wa kuendesha gari.😭😭😭😭😭 Niliogopa sana kuendesha gari bado siati gari sina. Nilikuwa kwa minyororo ya miaka mingi sana hata sikuweza kulala usiku kwa giza wakati fulani.

Tazama kanda ifuatayo;