Tume ya kuajiri walimu TSC yapandisha daraja walimu 16,152

TSC CEO Nancy Macharia
TSC CEO Nancy Macharia

Tue ya kuajiri walimu nchini, TSC imepandisha daraja walimu 16,152 baada ya kufanya mahojiano kati ya Desemba 2020 na Februari 2021, mkurugenzi Mtendaji Nancy Macharia ametangaza.

Katika ilani iliyotolewa Ijumaa jioni, Macharia alisema mahojiano hayo ni sehemu ya mwisho wa mkataba wa majadiliano ya Pamoja ya 2017-2021.

"Barua kuhusu matokeo ya mahojiano yako katika mchakato wa kutumwa kwa walimu wote ambao walihojiwa," alisema.

Miongoni mwa wale ambao wamepandishwa vyeo ni waalimu ambao watatumika kama Naibu mkuu 1 (T-Scale 13- D3), Naibu Mkuu II (T-scale 12, D2), Mhadhiri Mwandamizi I (T-scale 12, D2), Naibu Mkuu III (T-Scale 11-D1), Maafisa wa Usaidizi wa Mitaala (T-scale 10-C5)

Walimu wakuu (T-scale 10, C5), Senior Master IV (T-scale 9C4), Naibu Walimu Wakuu II (T-scale 9-C4), Mhadhiri Mwandamizi IV (T-scale 9-C4)  na walimu katika Master Senior I (T Scale 9- C4) vikundi vya kazi.

Wengine waliopandishwa vyeo ni pamoja na walimu wakuu na naibu walimu wakuu II, Mwalimu wa Sekondari I na II wanahudumu chini ya Miongozo ya Maendeleo ya Kazi na wale walio katika maeneo ya ASAL.

Macharia alizidi kuonya walimu dhidi ya kuwindwa na wadanganyifu wanaodai kuwa na uwezo wa kushawishi matokeo ya mahojiano hayo.

Mwaka jana, Chama cha Kitaifa cha Walimu cha Kenya kilipinga mpango wa kupandisha daraja  walimu 15,000 mnamo Januari 2021.

Katibu mkuu wa Knut Wilson Sossion alisema mawakili wa muungano huo watawakilisha kesi ya dharau dhidi ya TSC kwa kupuuza mipango ya utumishi.