Mbunge Ndindi Nyoro apigwa marufuku bungeni

Muhtasari
  • Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amepigwa marufuku bungeni kwa siku nne kutokana na hulka yake bungeni wakati wa mjadala kuhusu BBI
nyoro
nyoro

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amepigwa marufuku bungeni kwa siku nne kutokana na hulka yake bungeni wakati wa mjadala kuhusu BBI.

Spika mnamo Alhamisi alisema mwanachama yeyote alikuwa na uhuru wa kutoa hoja ya kusimamishwa kwa mwanachama huyo.

Spika Muturi hata hivyo alimwondolea mashtaka mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria baada ya yule wa pili kukana akisema wabunge walihongwa ili kupiga kura kwa BBI.

Hilo lilikemewa na wenzake wa mrengo wa handisheki na kutaka achukuliwe hatua kali kwa madai ya kukosea bunge heshima.

Mbunge atazuiliwa kutoka kwa viunga vya Bunge, pamoja na ofisi yake kwa siku nne. Muturi aliwahimiza wabunge kutendeana kwa heshima na kuepusha visa ambavyo vinadharau mwanachama yeyote.

"Matamshi yoyote ambayo yanamdharau mwanachama hayamuathiri tu mwanachama bali Bunge lote. Usingependa kuwa sehemu ya Bunge lenyewe ambalo umekosea kwa msimamo wao," Spika alisema.

Nyoro alitoa matamshi hayo wakati wa Muswada wa Marekebisho ya Katiba, kura ya 2020 Alhamisi iliyopita.

Kiongozi wa zamani wa wengi Aden Duale alimuuliza Nyoro kuchukua masomo kutoka kwa Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi ambaye alisimamishwa kazi mnamo 2015 kwa kuongoza maandamano ya filimbi katika hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta.