ULAGHAI MITANDAONI

Maelfu ya Wakenya walia kulaghaiwa mitandaoni

Wakenya wahofiwa kupoteza mamillioni waliowekeza kwenye mpango wa 'Amazon Web Worker'

Muhtasari

•Mitandao ya kijamii ilitumika kama chambo cha kushawishi wengine kujiunga

•Wakenya walichukua mikopo ili kuwekeza

Amazon Web Worker
Amazon Web Worker
Image: Hisani: Facebook

Kikundi kikubwa cha Wakenya  kinalia kulaghaiwa baada ya kuwekeza kwenye mpango wa kimtandao uliojulikana kama 'Amazon Web Worker.'

Mpango huo ulikuwa umepata umaarafu mkubwa mno nchini huku maelfu ya Wakenya wakiabulia  kwenye mtego huo ambao kwa sasa umetolewa kwenye programu ya Play Store. Maafisa waanzilishi walioonekana kusimamia shughuli hiyo pia hawapatikani tena tangu mwisho wa wiki iliyopita.

Mpango wa Amazon Web Worker haumo tena kwenye Play Store
Mpango wa Amazon Web Worker haumo tena kwenye Play Store
Image: HISANI

Inaripotiwa kuwa baadhi ya Wakenya huenda wakawa wamepoteza mamillioni ya pesa baada ya kuwekeza kwenye mpango huo ambao uliingiza mizizi yake nchini mnamo mwezi wa Mechi. Waliotangulia kujiunga na mpango huo wamekuwa na bidii mno kuwashawishi marafiki zao kujiunga pia huku wakiahidiwa marupurupu ya kuongeza wateja kwenye shughuli ile.

Mpango huo ulikuwa umewaahidi Wakenya kuwa wangekuwa wanapokea asilimia fulani ya pesa wanazowekeza kila siku. Pesa zaidi mtu angeliwekeza ndivyo marupurupu ya wanapokea kila siku yangekuwa mengi.

Hata hivyo, programu hiyo inadaiwa kutolewa kwenye programu ya Playstore na kisha maafisa wake kugura kutoka vikundi vilivyokuwa vinajumuisha waliokuwa wamejiunga na mpango huo mtandaoni.

"Amazon ni kesi iliyofungwa. Niko kwa vikundi zote na maafisa wote wamejitoa na kutungia njia zote za kuwafikia" Mtumizi wa Facebook kwa anayejitambulisha kama Lynne Mwangi aliandika kwenye kikundi cha AMAZON WEB WORKER KENYA kwenye mtandao huo wa Facebook

Waliokuwa kwenye mpango huo walikuwa wanatumia mitandao ya kijamii kujulishana na kushawishiana wenzao kujiunga wakiahidiwa utajiri mkubwa. Baadhi ya Wakenya waliendelea kutoa hisia zao na kukiri namna walikuwa wameanguka kwenye mtego huo laghai.

Hizi hapa baadhi ya hisia zilizotelewa na Wakenya kwenye mtandao wa Twitter.

"Elfu kumi na mbili zangu zimeenda hivyo tu. Nilijiunga na Amazon tarehe kumi mwezi wa Mei baada ya kuchukua mkopo wa Sh 25000 na nikawekeza sh20000 na kununua mpango wa shilingi elfu tano. Zimeenda zote." Mtumizi mwingine wa Facebook kwa jina Vero Muraya aliangika kwenye kikundi hicho.

Ujumbe wa Vero Muraya
Ujumbe wa Vero Muraya
Image: Hisani

Wamo baadhi ya waliojipata kwenye mpango wa Amazon wanaodai kuahidiwa kurejeshewa pesa zao mnao siku ya Jumanne na kwa sasa wanaishi kwa matarajio tu ila kulingana na Wakenya waliokuwa wamejipata kwenye ulaghai kama huo nafasi ya wao kupata pesa zao ni finyu sana.

Sio mara ya kwanza Wakenya wannajipata kwenye ulaghai  mitandaoni kwani mara kwa mara mipango kama ile hujitokeza ikiwemo mmoja ambao uliwapata wengi mwakani 2017 ulitambulika kama ‘Public likes’