Serikali kukusanya chanjo ambazo hazijatumika

MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Serikali imeanza kukusanya  dozi za chanjo ambazo hazijatumika kote nchini inapopanga kuanza kusambaza dozi ya pili juma lijalo.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema dozi hizi zitatumika pamoja na nyingine elfu 130 kutoka kwa kituo cha Covax. Amewataka wafanyikazi walio kwenye mstari wa mbele kuhakikisha wanapata dozi hiyo pindi watakapoarifiwa  kupitia mfumo wa chanjo.

Hayo yakijiri, umetakiwa kuhakikisha mwanao aliye chini ya miaka mitano anachanjwa dhidi ya polio katika zoezi la kuchanja linaloanza hii leo na linalolenga kuwafikia zaidi ya watoto milioni 3 humu nchini. Mkurugenzi wa afya kwa umma Francis Kuria anasema zoezi hilo la wiki moja litatekelezwa katika kaunti za Garissa, Isiolo, Kajiado, Kiambu, Kilifi, Kitui, Lamu, Machakos, Mandera, Naiorbi, Tana River and Wajir counties. 

Kwingineko, zaidi ya wahudumu 68  haramu wa zahanati wamekamatwa na kushtakiwa katika eneo la magharibi humu nchini  kwa kuhudumu kinyume cha sheria. Katika operesheni iliyoongozwa na bodi ya famasia nchini  na polisi makatoni 133 ya dawa tofauti yalinaswa huku zaidi ya maduka 114 ya dawa yakifungwa.