Covid-19: 324 waambukizwa huku 10 wakipoteza maisha yao

Hii leo watu 324 wamepatikana na virusi vya Covid-19 kutokana na sampuli 4,392 zilizopimwa masaa 24 iliyoisha.

Kutokana na visa hivyo, 298 ni wakenya huku 26 wakiwa wageni. 233 ni wanaume na 101 ni wagonjwa wa kike.

Mgonjwa mchanga zaidi ana mwaka mmoja huku mkonhwe zaidi akiwa na miaka 91.

Kufikia sasa ni visa 168,432 vilivyoripotiwa kutokana na sampuli 1,781,426.

Wagonjwa 85 wamepata nafuu kutokana na ugonjwa huo huku idadi ya waliopona ikifikia 114,537.

Katika habari za tanzia ni kuwa watu 10 wameaga na kufikisha idadi ya walioaga kupitia virusi hivyo kufikia 3,059.

Hata hivyo, kufikia sasa idadi ya watu 953,954 wamechanjwa kufikia sasa dhidi ya Covid-19 nchini kote.