MSIBA KAYOLE

Msichana, 8, wa gredi 2 aanguka na kufariki akijibu swali la hesabu

“Kule hospitali nilipata madaktari kama sita hivi wakaniuliza nguo ambazo mtoto wangu alikuwa amevaa na baada ya kuwaambia wakafungua pazia nikaona mwili wa mtoto wangu ukiwa umelala tuli” mama ya mtoto alisema

Muhtasari

•Jeniffer Ouma alikuwa mwanafunzi wa daraja ya pili katika shule ya msingi ya New View

•Jeniffer alipoanguka, walimu walimueka kwa chumba tofauti wakitumai kuwa angerejesha fahamu 

Linda achieng, mamake marehemu akiomboleza
Linda achieng, mamake marehemu akiomboleza
Image: Hisani: Star

Binti mmoja wa miaka nane alianguka na kufariki aliposimama kujibu swali la hesabu katika shule ya msingi ya New View iliyo Kayole.

Waalimu walisema kuwa Jeniffer Ouma ambaye alikuwa katika daraja la pili alianguka alipokuwa anajibu swali siku ya jumatano wiki iliyopita.

Jeniffer alipoanguka,  walimu walimueka kwa chumba tofauti wakitumai kuwa angerejesha fahamu badala ya kumpeleka hospitali.

Baada ya saa moja, mwanafunzi huyo bado hakuwa ameamka na ndipo akapeolekwa katika hospitali ya Mama Lucy na wanaume watatu wanaosemekana kaacha mwili huko baada ya kugundua kuwa Jeniffer hakuwa amerejesha nafuu.

Alitangazwa kafariki pindi tu alipofikishwa hospitali.

Maafisa wa polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini kama kuna uhalifu wowote uliofanyika kuhusiana na kifo hicho. Mwili wa marehemu utafanyiwa uchunguzi ili kusaidia katika kesi hiyo.

Mamake marehemu, Linda Achieng alisema kuwa aliitwa na maafisa wa polisi kuarifiwa kuwa mwanawe hakuwaa anahisi vizuri na amekimbizwa hospitali.

“Kule hospitali nilipata madaktari kama sita hivi wakaniuliza nguo ambazo mtoto wangu alikuwa amevaa na baada ya kuwaambia wakafungua pazia nikaona mwili wa mtoto wangu ukiwa umelala tuli” Achieng alisema.