'Raila ni rafiki yangu wa karibu,'Oscar Sudi asema baada ya kukutana na Raila Junior

Muhtasari
  • Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, siku ya Jumatano alikutana na mwanawe kinara wa ODM Raila Odinga nyumbani kwake
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter mwanasisa huyo alisema kwamba walijadili mambo mengi

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, siku ya Jumatano alikutana na mwanawe kinara wa ODM Raila Odinga nyumbani kwake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter mwanasisa huyo alisema kwamba walijadili mambo mengi.

Oscar ambaye ni  mfuasi sugu wa naibu rais William Ruto, alisema kuwa kinara wa ODM ni rafiki yake wa karibu.

Inafahamika vyema kwamba Raila na naibu rais na wafuasi wake Ruto hawajakuwa wakisikizana kwa muda huku wakipena maneno makali kati yao.

Pia pande hizo mbili zimekuwa zikikosoana au kukashifiana hadharani, kwa muda sasa uvumi umeenea kwamba kinara wa ODM na naibu rais wataungana mikono mnamo mwaka wa 2022 wakati wa uchaguzi mkuu.

"Leo asubuhi nimemkaribisha rafiki yangu @Railajunior katika nyumba yangueneo la Kapseret. Tulikuwa na mazungumzo yenye mafanikio juu ya mambo kadhaa

Tunatarajia kuwa na mikutano kama hiyo ili kuimarisha uhusiano wetu wa kifamilia ukizingatia hilo @RailaOdinga pia ni rafiki yangu wa karibu," Aliandika Sudi.

Swali kuu ni je kinara wa ODM Raila Odinga na naibu rais William Ruto wataungana na kuja pamoja mwaka wa 2022?