DP Ruto awataka viongozi kumaliza uhasama baina yao

Muhtasari
  • DP Ruto awata viongozi kumaliza uhasama baina yao
  • Ruto alikumbuka ujumbe wa kinara wa ODM Raila Odinga kwenye hafla ya maombi miaka miwili iliyopita
Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
William Ruto Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
Image: DPPS

Naibu Rais William Ruto amewataka viongozi humu nchini kumaliza uhasama baina yao na kuanza kutafuta suluhu ya matatizo ya Kenya.

Akiongea wakati wa hafla ya maombi kwa taifa iliyofanyika katika majengo ya bunge, Ruto alisema janga la coronavirus ni ujumbe kwa viongozi kufanya kazi pamoja.

"Mambo mengi yamefanyika, lakini hii leo ziara za Tangatanga zimesimama sawa na reggae iliyokuwepo. Nafikiri ni wakati tuskize ujumbe kuwa tunafaa kufanya kazi pamoja," alisema Ruto.

Ruto alikumbuka ujumbe wa kinara wa ODM Raila Odinga kwenye hafla ya maombi miaka miwili iliyopita.

Kwenye hotuba yake, Ruto alisherehekea kuteuliwa kwa Martha Koome kama Jaji mkuu mwanamke wa kwanza na kumpongeza kwa uteuzi huo. Pia alimpongeza spika wa bunge la kitaifa, Justin Muturi kwa kutawazwa kuwa msemaji wa eneo la Mlima Kenya.

Naibu rais pia alisisitiza kuwa wakati umefika wa viongozi kufanya kazi pamoja huku akisema kuwa kusimama kwa ziara za tangatanga na kutupiliwa mbali kwa mchakato wa BBI kuwa ni ishara kuwa Mungu anawataka viongozi kuwaza pamoja.

"Aliyekuwa kinara wa ODM alitukumbusha kuhusu Isaya 1:18 inayosema 'Njooni, basi, tuhojiane,' ni kama Mungu anatuita akisema tukae pamoja,'Ruto Alizungumza.