DP Ruto,Raila Odinga wawaongoza wakenya kumuomboleza Kalembe Ndile

Muhtasari
  • William Ruto,Raila Odinga wawaongoza wakenya kumuomboleza Kalembe Ndile
kalembe.ndile.
kalembe.ndile.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amewaongoza Wakenya kumuomboleza aliyekuwa Mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile.

Ndile aliaga dunia akipokea matibabu katika  Hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuhangaika na ugonjwa wa ini.

"Kwa mshtuko mkubwa, nimejifunza juu ya kufariki kwa mbunge wa zamani .. Watu wa Kibwezi na nchi yetu wamepoteza kiongozi mwenye haiba,

.. na ustadi wa kipekee wa uhamasishaji wa watu wa chini ambao pia aliwajali sana wale walio chini. pumzika kwa Amani ya Milele." " Raila alisema.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amesema amehuzunishwa sana kujua juu ya kufariki kwa mmoja wa wasemaji wakuu wa kisiasa nchini Kenya "Mtoto wa Squatter".

"Ndile alikuwa sauti jasiri ya watu. Kiongozi aliyejitengeneza, alikuwa kipenzi kwa hadhira na kwetu sote. Hasara kubwa kwa mkoa wetu. Kenya imepoteza shujaa," alisema.

Kioko, mtoto wa Kalembe Ndile, alithibitisha kifo cha baba yake.PIa gavana wa kaunti ya Kisumu Wycliffe Oparanya alimuomboleza Kalembe ambae alisema alikuwa mwanasiasa aliyekuwa na bidii katika kazi yake.