Rais Uhuru, DP Ruto na Raila wawafurahisha wakenya baada ya kusakata densi siku ya Madaraka

Muhtasari
  • Rais Uhuru, DP Ruto na Raila wawafurahisha wakenya baada ya kusakata densi siku ya Madaraka 

Wanamtandao  na wakenya ambao wanaangalia vizuri Sherehe za Madaraka katika uwanja wa Kimataifa wa Kisumu Jomo Kenyatta kwa mara ya kwanza tangu Uhuru wa kenya , walipendezwa na jinsi baadhi ya wanasiasa walisakata densi wakati wa burudani.

Wakati wa sehemu ya burudani, mkuu wa nchi alionekana akitikisa kichwa kwa raha.

Lakini wakati wa utendakazi wa nyota wa Benga Osito Kalle Kasam, mkuu wa nchi hakuweza kuishikilia tena, alisimama na kuanza kusakata densi.

Huku akiwa amevalia suti nyeusi, shati jeupe na tai nyekundu, Uhuru alipiga viwiko vyake kwa wimbo na huku akipiga makofi mara kwa mara.

Viongozi wengine akiwemo Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga na Gavana wa Kisumu Anyang 'Nyong'o, walijiunga naye kwenye densi.

Kutoka kwetu wanajambo tunawatakia mashabiki wa Radiojambo, sikuu njema wanaposheherekea sikukuu ya Madaraka.