KILIO CHA WANAUME EMBU

Embu: Wanaume walalamikia kupigwa na mabibi na kunyimwa haki za ndoa

Wamesema kuwa kila wanapopiga ripoti kwa maafisa wa polisi kuhusu kutendewa vibaya wanadharauliwa na kufukuzwa huku wakiitwa waoga

Muhtasari

•Walilalamika kuwa majukumu yao kwa familia yalikuwa yametupiliwa mbali  na hawakuwa tena kwenye usukani .

•Wamelaumu u utumizi wa madawa ya kulevya miongoni mwa vijana kuwa sababu moja ya matatizo yale.

Kiongozi wa kikundi cha InuaWazee Joseph Wega akiwa kwenye mkutano Kiriari, Embu siku ya Jumanne
Kiongozi wa kikundi cha InuaWazee Joseph Wega akiwa kwenye mkutano Kiriari, Embu siku ya Jumanne
Image: The Star

Wanaume walio kwenye ndoa katika kaunti ya Embu wamelalamikia kile wanachosema ni kukandamizwa na wake na watoto wao.

Wametaja kupigwa, kunyimwa haki za ndoa na kupigwa vita baridi kwenye familia kama baadhi ya shida wanazopitia kwenye boma zao.

Wanachama wa Inua Wazee Self Help Group upande wa Kiriari, Embu ya Kaskazini wameomba serikali kuingilia kati huku wakilaumu utumizi wa madawa ya kulevya miongoni mwa vijana kuwa sababu moja ya matatizo yale.

Wanachama hao wamesema kuwa kila wanapopiga ripoti kwa maafisa wa polisi kuhusu kutendewa vibaya wanadharauliwa na kufukuzwa huku wakiitwa waoga. Walilalamika kuwa majukumu yao kwa familia yalikuwa yametupiliwa mbali  na hawakuwa tena kwenye usukani .

Wanaume wametengwa na htuonekani kuwa wa maana tena. Wanawake wamechukua usukani na hatuna nguvu tena. Hatuwezi piga ripoti kwa wanapolisi na kila tunapojaribu kujipigania maafisa wa polisi wanatuchukulia hatua kali” Kiongozi wa InuaWazee, Joseph Wega alisema.

Alieleza kuwa hali hiyo ilikuwa imewavunja moyo wanaume wengi na kusababisha wengine kujiua.

“Tunapitia shida mingi kwenye familia zetu na hatuwezi furahia ndoa. Tunaomba serikali kuwawezesha wanaumena kufanikisha usawa kwa  wanawake na wanaume katika kaunti hii” Mwanachama wa InuaWazee, Samuel Muturi alisema.

Wanaume walitengeneza kikundi ili kuwaleta pamoja na kuwa na sauti iwapo mmoja wao anapitia matatizo kwenye familia.

Nahimiza wanaume katika kaunti ya Embu kuunda vikundi ili wapate nguvu za kufanya sauti yao isikike. Hili litawaruhusu haki za wanaume kuangaziwa” David Murage alisema.

(Tafsiri na Samuel Maina)