logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ed Sheeran kucheza kibao kipya katika Tamasha la Euro

Tamasha hilo litafanyika kutoka nyumbani kwa msanii huyo mjini Ipswich tarehe 25 Juni na kuonyeshwa bure kupitia mtandao wa TikTok

image
na Radio Jambo

Habari04 June 2021 - 10:44

Muhtasari


•Kombe la EURO 2020 lilifaa kuchezwa mwaka jana ingawa liliahihirishwa kutokana na  janga la Corona.

•Ed Sheeran alitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa akisaidiana na aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United na ambaye ni mmiliki wa klabu ya Inter Miami David Beckham.

Ed Sheeran

Mwanamuziki wa nyimbo za pop, Ed Sheeran ametangaza kuwa atacheza kwenye tamasha ya Tiktok UEFA EURO 2020 usiku wa Juni 25.

Tamasha hilo litafanyika nyumbani mwa msanii huyo maeneo ya Portman Road mjini Ipswich, Uingereza na  kuonyeshwa bure kupitia mtandao wa TikTok.

Ed Sheeran alitoa tangazo hilo siku ya Ijumaa akisaidiana na aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United na ambaye ni mmiliki wa klabu ya Inter Miami David Beckham.

Sheeran pia  atakuwa akizindua kibao kipya kwenye tamasha hiyo.

Siwezi ngoja kucheza katika tamasha la TikTok UEFA EURO 2020 kutoka Portman Road. Ni mahali napenda na natazamia sana kucheza ngoma kadhaa ambazo mashabiki wanapenda na pia kibao change kipya kwa mara ya kwanza “ Sheeran alisema.

Kampuni ya TikTok ilitangazwa kuwa mdhamini wa kwanza wa kombe la EURO 2020 mapema mwaka huu.

Kombe hilo ambalo lilifaa kuchezwa mwaka jana liliahihirishwa kutokana na  janga la Corona.

Mechi ya kwanza kwenye kombe hilo itakuwa kati ya Uturuki na Italia tarehe 11 Juni huku fainali ikitarajiwa kuchezwa tarehe 11 mwezi wa Julai.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved