DRAMA KITUI

Kitui: Nyoka aanguka toka kwenye makucha ya tai na kuuma dereva

Tai yuleyule alimchukua tena nyoka huyo aina ya black mamba baada ya kuuliwa na kutoweka juu angani

Muhtasari

•Wakazi wa Kwa Mbugu, Kitui walibaki na mshangao na wasiwasi kutokana na kile walichokiita tukio la kiuchawi.

David Musyoka akiwa hospitalini
David Musyoka akiwa hospitalini
Image: The Star

Mwanaume mmoja kwa jina David Musyoka aliumwa na nyoka  iliyoanguka ndani ya gari lake kutoka mdomoni mwa tai.

Nyoka huyo aina ya Black Mamba aliangushwa kwenye paa la gari yake na tai aliyekuwa amembeba kisha akatambaa hadi ndani mwa gari lake na kumuua kwenye mkono wake wa kushoto.

Musyoka ambaye ni mkazi wa Mutito, Kitui ya Mashariki alisema kuwa alisimamisha gari ghafla huku nyoka yule akiwa ananing’inia toka kwa mkono wake .

Wakazi wa soko ya  Kwa Mbungu, Mwingi ya Mashariki walikimbia kumsaidia punde alipopiga nduru na kuanza kumuua nyoka yule.

Wengine walimakinika kumuua nyoka yule huku wengine wakiharakisha kunipatia huduma ya kwanza” Musyoka alisema.

Hadithi yaendelea kutatanisha:

Nyoka yule alichukuliwa tena na tai kisha akapaa juu kabisa kwenye anga” Musyoka alisimulia.

Musyoka alikimbishwa katika hospitali ya Mwingi Level 4 ambako alihudumiwa na kupewa ruhusa. Madaktari wanasema kuwa anaendelea vyema.

Wakazi wa Kwambugu, Kitui walibaki na mshangao na wasiwasi kutokana na kile walichokiita tukio la kiuchawi.

Beth Kituo alieleza The Star kuwa huenda nyoka yule alitumwa kuua mwanaume yule. Alihimiza watu wawe waumini kwani matendo kama yale yanahusishwa na uchawi.

"Ni jambo la kutatanisha sana kwani baada ya nyoka kuuliwa alichukuliwa na tai yule yule na kutoweka" Musyoka alisema

(Tafsiri na Samuel Maina)