Makali ya corona: Idadi ya visa vya maambukizi ya corona imefika 173,661

Muhtasari
  • Watu 589 wapatikana na corona,19 waaga dunia
  • Kati ya visa hivyo vipya 580 ni wakenya ilhali 9 ni raia wa kigeni,343 ni wagonjwa wa kiume huku 246 wakiwa wa kike
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 5 ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 101

Visa  589 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini siku ya JUmatano kutoka kwa sampuli 4,995 na kufkisha idadi jumla ya 173,661 vya maambukizi ya maradhi hayo.

Kati ya visa hivyo vipya 580 ni wakenya ilhali 9 ni raia wa kigeni,343 ni wagonjwa wa kiume huku 246 wakiwa wa kike.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 5 ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 101.

Kaunti ya Kisumu imerekodi visa 100,Nairobi visa 91 huku Bungoma ikiwa na visa 60 siku ya Jumatano.

Kulingana na wizara ya afya watu312 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 118,933 ya watu waliopona corona.

184 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 128 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hopitali mbalimbali nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha ni kuwa watu 19 wameaga dunia kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,345 ya watu walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 994 ambao wamelazwa hospitalini, huku 5,049 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Vile vile wagonjwa 114 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).