Mchina aliyehusika kwenye vita na mfanyakazi apigwa kalamu

Kufuatia tukio hilo, kampuni ya reli ya China Railways Seventh Group(CRSG) imetoa ujumbe ikitangaza kuwa Mchina yule alikuwa ameachishwa kazi.

Muhtasari

•Mchina huyo ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya CRSG alionekana kuendea chuma ambayo alitumia kumdunga nayo mfanyakazi huyo kwenye sehemu zake za siri.

•Mfanyakazi huyo kwa ghadhabu alionekana kulipisha kisasi kwa kumpiga Mchina huyo teke aina ya 'drop kick 'na kumuangusha sakafuni.

Kwa kipindi cha siku kadha zilizopita, video inayoonyesha vita kati ya Mchina na mfanyakazi wa nchi ya Sierra Leone imekuwa ikisambaa sana mitandaoni.

Kwenye video hiyo, Mchina anaonekana akimchokoza mfanyakazi mmoja wa  kampuni ya Kingho aliyekuwa anasoma ripoti. Mfanyakazi huyo kwa hasira anaonekana kumtupia teke Mchina huyo na hapo vita kubwa inaibuka kati ya wawili hao.

Mchina huyo ambaye ni mwajiriwa wa kampuni ya CRSG alionekana kuendea chuma ambayo alitumia kumdunga nayo mfanyakazi huyo kwenye sehemu zake za siri.

Mfanyakazi mmoja kati ya waliokuwa wanahuhudia vita hiyo alionekana kujaribu kutenganisha vita ile.

Hata hivyo, mfanyakazi huyo ambaye  alikuwa amejawa na ghadhabu kutokana na kudungwa na Mchina yule alionekana kulipisha kisasi kwa kumpiga Mchina huyo teke aina ya 'drop kick 'na kumuangusha sakafuni.

Kufuatia tukio hilo, kampuni ya reli ya China Railways Seventh Group(CRSG) imetoa ujumbe ikitangaza kuwa Mchina yule alikuwa ameachishwa kazi.

Kwenye ujumbe huo uliotolewa siku ya Jumatano, CRSG imeomba msamaha kutokana na tukio hilo huku ikiahidi kuwa halitatokea tena.

"Vita kati ya Mchina mfanyakazi wa CRSG na mfanyakazi wa kampuni ya Singho raia wa Sierra Leon kataika duka letu la ufundi kwenye upande wa Tonkoli kama ilivyoonyeshwa kwenye video iliyoenea mitandaoni haikutarajiwa na ni kesi iliyotengwa." Kampuni hiyo iliandika.

Maoni ya CRSG ni kuwa tabia ya Mchina huyo haikubaliki na ni mbaya. Bila kuangazia kilichoibuka, CRSG ingependa kuomba msamaha kutokana na tukio hilo la lisilo nzuri na imeamua kumuachisha kazi Mchina huyo mara moja” Kampuni hiyo ilisema

Kwa ujumbe mwingine uliotolewa sikuya Ijumaa, kampuni hiyo ilitangaza kuwa ilikuwa imesuluhisha mgogoro kati ya wawili hao.

"CRSG imesuluhisha mgogoro kati ya mfanyakazi wake na mfanyakazi wa kampuni ya Kingho kufuatia vita iliyoshuhudiwa katika duka moja pande ya Tonkolili. CRSG  Inawahitaji wafanyakazi wake kutii sheria za nchi na inatumai kuwa tukio kama hilo halitatokea tena" CRSG iliandika.