Nilikataliwa shule kwa ajili ya ualbino-Isaac Mwaura asema

Muhtasari
  • Isaac Mwaura aeleza jinsi alikataliwa shule kwa ajili ya Ualbino
  • Wamekuwa wakipitia changamoto tofauti na hatakukataliwa na jamaa zao na marafiki zao
  • Ulimwengu utaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Wa Ualbino Jumapili, Juni 13
Isaac Mwaura
Image: Maktaba

Watu wenye ualbino hukumaba na madhila mengi haswa nchini kenya kwani wengi hawajaelimishwa jinsi ya kuishi na watu wenye ualbino.

Wamekuwa wakipitia changamoto tofauti na hatakukataliwa na jamaa zao na marafiki zao.

Ulimwengu utaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Wa Ualbino Jumapili, Juni 13.

Huku alyekuwa seneta mteule Isaac Mwaura akiwa kwenye mahojiano alizungumzia changamoto ambazo alikumbana nazo alipokuwa anakua.

Na jinsi alibaguliwa, hata kukataliwa shule kwa ajili ya rangi ya ngozi yake.

"Nilikulia katika mazingira magumu kwa sababu watu waliokuwa karibu nami walikosa ujuzi wa Ualbino. Nilizaliwa tofauti kati ya wanafamilia yangu

Familia yangu haikuelewa kwanini ngozi yangu ilikuwa tofauti, baba yangu aliondoka, kwa hivyo nililelewa na mama yangu peke yake. Alisema hawezi kumzaa mtoto ambaye anaonekana kama nguruwe.

Maneno hayo yalikuwa machungu sana. Nilikuwa nikilazwa kwenye jua na ningepata kuchomwa na jua. Mama yangu hangeweza kununua jua. Nilipelekwa kwa KNH kwa matibabu.

Nililazimika kuandikishwa katika shule ya kitalu katika miaka 4 na nusu. Kulikuwa na shule moja tu huko Kiambu ambayo ilikuwa ikidahili watoto kama mimi. "Mwaura alizungumza.

Mwaura, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ualbino nchini Kenya pia amekabiliwa na ubaguzi kutoka kwa wanasiasa wenzake kwa sababu ya rangi yake ya ngozi.

"Katika shule ya upili, nilikuwa nimechaguliwa kujiunga na  shule ya wavulana ya Starehe lakini walikataa kunikubali kwa sababu ya rangi yangu ya ngozi."