Wooishe chama cha Jubilee kwenye shida-Moses Kuria asema baada ya kupakia video hii

Muhtasari
  • Moses Kuria adai chama cha JUbilee kiko kwenye shida baada ya kupakia video ya mwanamke akisifia chama cha UDA
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria akizungumzia wanahabari katika eneo bunge la Kiambaa siku ya Jumapili
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria akizungumzia wanahabari katika eneo bunge la Kiambaa siku ya Jumapili
Image: Facebook

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ni mmoja wa viongozi ambao walijitenga na chama cha jubilee.

Katika kipindi cha pili katika ofisi, uhusiano kati ya naibu Rais William Ruto na Rais Uhuru walipunguahuku wengi wakidai kwamba ndoa kati ya vigogo hao wawili imevunjika.

Viongozi wengine walikwenda upande wa DP Ruto wakati wengine walibakia upande wa Rais Uhuru.

Vigogo hao wamekuwa wakishambuliana kwnye mitandao ya kijamii na hata kwenye mikutano huku wengi wakimkosoa rais Kenyatta.

Baadhi ya viongozi walidai kwamba uhusiano kati ya rais na naibu wakee ulidhoofika baada ya Uhuru kuungana na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Kupitia kwenye ukurasa wake Kuria wa facebook alipakia video ya mwanamke akiwa amevalia kikoi cha chama kinachohusishwa na naibu rais UDA.

Mwanamke huyo alikuwa anasakata densi, Kuria alipakia video hiyo na kuandika kwamba chama cha JUbileee kiko kwenye shida.

"Wooishe chama cha jubilee kiko kwenye shida," Aliandika KUria.

Hii ina maana kwamba Kuria alifurahi kwa ajili ya mwanamke huyo, na jinsi Jubilee haikupokea sifa.

Swali kuu ambalo limesalia akilini mwa wananchi katika uchaguzi mkuu ni chama kipi kitakachoshinda?

Hii hapa video hiyo;

Wooishe Jubilee is in trouble

Posted by Moses Kuria on Sunday, June 13, 2021