Baba aliyeruhusu mwanawe wa miaka 7 kuendesha gari barabarani akamatwa

Kukamatwa kwa Kinyajui kulitokana na video iliyovuma sana mitandaoni siku za hivi karibuni ikionyesha mtoto mdogo akiendesha gari aina ya Prado TX kwenye barabara moja pande za Gatanga.

Muhtasari

•Ayub Kinyajui Mungai anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne na kukabiliwa na shtaka la kuruhusu mtu ambaye hana leseni halali kuendesha gari.

Gari alilokuwa anaendesha Ryan
Gari alilokuwa anaendesha Ryan
Image: Hisani

Maafisa wa polisi upande wa Murang’a wanazuilia mwanaume mmoja aliyeruhusu mtoto wake wa miaka 7 kuendesha gari kwenye barabara ya umma.

Ayub Kinyajui Mungai anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne na kukabiliwa na shtaka la kuruhusu mtu ambaye hana leseni halali kuendesha gari.

Kukamatwa kwa Kinyajui kulitokana na video iliyovuma sana mitandaoni siku za hivi karibuni ikionyesha mtoto mdogo akiendesha gari aina ya Prado TX kwenye barabara moja pande za Gatanga.

Kwenye video hiyo, mtoto aliyejitambulisha kama Ryan anaonekana akiwa amekalia kiti cha dereva huku ameshika usukani. Mwanaume mmoja anasikika akimhoji ikiwa kweli ni yeye anaendesha gari lile huku akirekodi video ya mazungumzo yale.

Mwanaume: Hey, habari yako

Ryan: Poa

Mwanaume: Unaitwaje?

Ryan: Ryan

Mwanaume: Je ni kweli ni wewe unaendesha gari hili?

Ryan: Naam

Mwanaume: Unaliendesha??

Ryan: Naam

Mwanaume: Haya basi endesha nione

Baada ya mahojiano hayo mafupi Ryan anaonekana kuendesha gari lile na kuenda kabisa.

Kinyajui alikamatwa na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kirwara wakishirikina na maafisa wa DCI kutoka Gatanga siku ya Jumatatu.

Kukamatwa