Daktari ajitia kitanzi ndani ya gari lake - KNH

Chupa mbili za dawa za kuzuia uchungu aina ya Ketamine na Midazolam pamoja na sindano ni baadhi ya vitu vilivopatikana kando ya mwili wa daktari Lydia Wahura Kanyoro, 35.

Muhtasari

• Marehemu alikuwa ameandika ujumbe ambao unadaiwa kuzungumzia maisha yake.

• Ujumbe huo unafanyiwa utafiti na maafiisa wa polisi.

Daktari Lydia Wahura Kanyoro
Daktari Lydia Wahura Kanyoro
Image: The Star

Huzuni imetanda ali baada ya daktari mmoja wa watoto katika Hospitali ya Kenyatta kujiua  akiwa ndani ya gari lake.

Mwili wa Lydia Wahura Kanyoro, 35, ambaye alikuwa mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Nairobi ulipatikana ndani ya gari lake lililokuwa limeegeshwa ndani ya hospitali na mkuu wa ulinzi katika chuo cha udaktari mwendo wa saa saba mchana siku ya Jumamosi.

Chupa mbili za dawa za kupunguza maumivu aina ya Ketamine na Midazolam  pamoja na sindano ni baadhi ya vitu zilizopatikana kwenye eneo hilo la tukio.

Mwili wa marehemu ulipatikana kwenye kiti cha nyuma ya gari.

Marehemu alikuwa ameandika ujumbe ambao unadaiwa kuzungumzia maisha yake. Ujumbe huo unafanyiwa utathmini na maafiisa wa polisi. Hata hivyo, polisi hawakufichua maandishi ya ujumbe huo kwa madai kuwa ni ushahidi muhimu kusaidia kwa upelelezi.

Mashahidi wameeleza kuwa walimuona Wahura akiingia darasani mida ya saa tatu mchana siku ya Jumamosi.

Dakika chache baadae, Wahura alionekana akitoka darasani na kuelekea kwenye gari lake

Wapelelezi kutoka kituo cha Kilimani na madaktari wenzake  wanafanya uchunguzi kubaini kilichomsukuma hadi kujitoa uhai.

Imeripotiwa  kuwa marehemu alikuwa amepigia baadhi ya jamaa zake kuwaeleza alikokuwa na alichotaka kufanya kabla ya kujiua.

Maafisa ambao walifika kwenye eneo la tukio walipata sindano tatu na dawa aina ya Ketamine na Midazolam ambazo zinafanyiwa uchunguzi kwene maabara ya serikali.

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa amezongwa na matatizo na alikuwa mwenye huzuni hali ambayo huenda ilichangia kujiua kwake.

Wahudumu wengi wa afya wamekuwa wakikabiliana na changamoto si haba kutokana na athari za janga la Covid-19. 

(Mhariri Davis Ojiambo).