Naogopa kufa, nahofia kuishi: Maneno ya mwisho ya daktari aliyejitia kitanzi

Nini kilichompelekea daktari aliye na nyota kubwa kujitia kitanzi?

Muhtasari

•Lydia alisema kuwa ilikuwa ngumu sana kuishi ndani ya ngozi isiyo yake na maisha hayakuwa jinsi alivyotarajia.

•Wenzake walimsema kuwa mtaalam shupavu na mwanafunzi bora aliye na nyota kubwa.

daktari lydia wahura kanyoro aliyejitia kitanzi
daktari lydia wahura kanyoro aliyejitia kitanzi
Image: Hisani

Daktari Lydia Wahura  Kanyoro, 35, alikatiza maisha yake kwa kujidunga na madawa ya kuzuia uchungu katika eneo la kuegesha magari kwenye hospitali ya Kenyatta.

"Poleni sana ila sitarajii kusamehewa. Naogopa kufa ila nahofia zaidi kuishi" ujumbe ambao mwanafunzi huyo wa shahada ya uzamili alikiuwa ameandika ulisoma.

Alisema kuwa ilikuwa ngumu sana kuishi ndani ya ngozi isiyo yake na maisha hayakuwa jinsi alivyotarajia.

Wenzake walimsema kuwa mtaalam shupavu na mwanafunzi bora aliye na nyota kubwa.

Maafisa wa polisi wanachunguza ujumbe wa kujiua ili kubaini kama kweli ni yeye aliyeandika ujumbe huo ambao unasemekana kuandikwa kwa mafumbo . Hata hivyo walisita kueleza zaidi kuhusu maandiko hayo wakidai kuwa na ushahidi muhimu.

Ujumbe huo ulikuwa umechapiswha kutoka kwa barua pepe iliyonakiliwa  saa tatu asubuhi, tarehe 12 mwezi Juni .

Upasuaji wa mwili ulifanyiwa Jumanne ili kuchunguza zaidi kuhusiana na kifo hicho.

Wahura alikuwa mwanafunzi wa shahada ya uzamili kwenye masomo ya udaktari  katika  tawi la chuo kikuu cha Nairobi lililoko katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Mwili wake ulipatikana siku ya Jumamosi mida ya saa saba mchana ukiwa kwenye kiti cha nyuma cha gari lake na kando yake palikuwa na chupa mbili za madawa ya kuzuia uchungu na sindano tatu.

Haijabainika wazi kilichompelekea saktari huyo kujiua.

Kifo chake kinaibua maswali kuhusiana na msongo wa mawazo baina ya wahudumu wa afya nchinini

Wapelelezi upande wa Kilimani na wahudumu wa afya wenzake wanafanya uchunguzi kubaini kilichomfanya Wahura kujitia kitanzi.

Msongo wa mawazo baina ya wahudumu wa afya umekita mizizi tangu mwanzo wa janga la COVID  19 ikisemekana kuwa uchovu na huzuni ni baadhi ya sababu zinazoleta tatizo hilo.

(Utafsiri na Samuel Maina)