MAAFA NAIROBI

Binti ya bosi wa polisi afariki baada ya kupondwa na matatu mbili

Matatu moja iliyokuwa inarudi nyuma ilimsukuma na kumponda kwenye matatu nyingine iliyokuwa imesimama

Muhtasari

•Inadaiwa kuwa alikuwa anavuka kutoka barabara maeneo ya Tom Mboya wakati ajali hiyo ilipotokea mida ya saa mbili asubuhi siku ya Alhamisi.

•Baada ya tukio hilo, Waithera alikimbizwa na gari la kubebea wagonjwa hadi hospitali kuu ya Kenyatta ila akaaga alipokuwa anahudumiwa kufuatia majeraha mabaya aliyokuwa amepata.

Crime scene
Crime scene

Hali ya huzuni kwenye familia ya mukubwa mmoja wa polisi  jijini Nairobi baada ya binti yake kupondwa na matatu mbili hadi kuaga

Nelly Waithera, 25, amabye ni binti ya naibu inspekta generali Edward Mbugua aliaga baada ya kupondwa kati ya matatu mbili kwenye kijia cha Murang'a jijni Nairobi.

Inadaiwa kuwa alikuwa anavuka kutoka barabara maeneo ya Tom Mboya wakati ajali hiyo ilipotokea mida ya saa mbili asubuhi siku ya Alhamisi.

Mmoja wa walioshuhudia tukio hilo alisema kuwa matatu moja iliyokuwa inarudi nyuma ilimsukuma na kumponda kwenye matatu nyingine iliyokuwa imesimama na kusababisha majeraha mabaya kichwani.

Baada ya tukio hilo, Waithera alikimbizwa na gari la kubebea wagonjwa hadi hospitali kuu ya Kenyatta ila akaaga alipokuwa anahudumiwa kufuatia majeraha mabaya aliyokuwa amepata.

Mwili wa marehemu ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Kenyatta huku upasuaji wa mwili ukisubiriwa.

Magari mawili yaliyohusika kwenye ajali hiyo yanazuiliwa katika kituo cha polisi.

Madereva wa magari hayo waliachiliwa huru baada ya kuhojiwa kwa muda. Maafisa wa polisi wameeleza kuwa kesi hiyo inashughulikiwa.

(Mtafsiri:  Samuel Maina)