ILIFANYIKA VIPI?

Mshangao baada ya Wakenya kugundua wamesajiliwa kwenye vyama vya siasa bila idhini

Imeibuka kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa imekuwa ikiwasajili Wakenya kwenye vyama tofauti vya kisiasa bila idhini yao.

Muhtasari

•Wakenya wengi wameeleza mshangao wao baada ya kuingia kwenye tovuti rasmi ya huduma za umma  na kupata kuwa wamesajiliwa kama wanachama wa chama fulani cha kisiasa. 

ORPP
ORPP
Image: Hisani

Huenda wewe ni mwanachama  rasmi wa chama fulani cha kisiasa nchini na huna fahamu!

Wakenya wengi wameendelea kueleza ghadhabu yao baada ya kugundua kuwa wamesajiliwa katika vyama vya kisaisa bila idhini.

Imeibuka kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa imekuwa ikiwasajili Wakenya kwenye vyama tofauti vya kisiasa bila idhini yao.

Kati ya vyama ambavyo wengi wameandikishwa ni pamoja na cha Jubilee, ODM na Amani National Congress. 

Wakenya wengi wameeleza mshangao wao baada ya kuingia kwenye tovuti rasmi ya huduma za umma  (orpp.ecitizen.go.ke ) na kupata kuwa wamesajiliwa kama wanachama wa chama fulani cha kisiasa. 

Wengi wameeleza ghadhabu yao kupitia mitandao ya kijamii. Hizi hapa baadhi ya hisia za Wakenya

Jua chama ulichosajiliwa kwa kuingia kwenye tovuti ya   (orpp.ecitizen.go.ke)