Iwapo Martha Karua atawania kama naibu wa Raila, Ruto ataona kivumbi-Mutahi Ngunyi

Muhtasari
  • Mutahi Ngunyi asema dawa ya Ruto ni Martha Karua
  • Mutahi amekuwa mkosaoji mkubwa wa naibu rais William Ruto
  • Pia alimshauri Karua na Raila waungane mnamo mwaka wa 2022 ili Ruto apate kivumbi
mutahi ngunyi
Mutahi Ngunyi mutahi ngunyi
Image: Maktaba

Kuna mwanaume mmoja pekee katika Mt Kenya ambaye anamuweza William Ruto. Na huyo mwanaume ni Martha Karua.

Haya na matamshi yake mchanganuzi wa saisa Mutahi Ngunyi aliyoyasema katika ukurasa wake wa twitter.

Ngunyi alisema Martha Karua na Raila Odinga wakiungana naibu rais hatapata nafasi ya mlima kenya wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Mutahi amekuwa mkosaoji mkubwa wa naibu rais William Ruto.

Pia alimshauri Karua na Raila waungane mnamo mwaka wa 2022 ili Ruto apate kivumbi.

“Kuna mwanaume mmoja pekee katika Mt Kenya ambaye anamuweza William Ruto. Na huyo mwanaume ni Martha Karua. Fikirie kuhusu hilo ,Iwapo Martha Karua atawania kama naibu wa Raila, Ruto ataona kivumbi au nimekosea kwa hili," Alisema Mutahi.